Kenya imethibitisha wagonjwa 30 wapya hatua inayoongeza idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini humo kufikia 465 kulingana na katibu wa kudumu katika wizara ya afya nchini humo Rashid Aman.

Kati ya wagonjwa hao wapya 19 wanatoka Momabasa , wanane kutoka Nairobi , wawili kutoka Bungoma na mmoja kutoka kaunti ya Kitui.

Hatahivyo wagonjwa 15 wameripotiwa kupona virusi hivyo vya corona huku wawili wakifariki na kufanya idadi yao kufikia 24.

  • Magufuli kutuma ndege Madagascar kufuata ‘dawa ya corona’
  • Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona
  • Je unaweza kupata maambukizi ya corona kutoka kwa mfu?

Kulingana na katibu huyo takriban sampuli 883 zilifanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24 na wagonjwa hao wapya ni wenye umri wa kati ya miaka 4 hadi 67.

Aman aliwataka Wakenya kuendelea kufuata muongozo wa serikali katika kukabiliana na virusi hivyo.

Amewataka Wakenya waliojitolea kupimwa virusi hivyo.

Baadhi ya hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta za kukabiliana na janga la corona

1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona

2. Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19

3. Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.

4. Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitafaidi kutokana na fedha zilizotengwa na serikali kusaidia familia zisizojiweza

5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.

6. Ili kuhakikisha msaada unagawanywa kwa njia salama, mfuko wa hali ya dharura wa kukabiliana na Covid-19, Kenya na mashirika mengine ya usalama yatashirikiana kuratibu miradi kama ule wa Adopt a Needy Family, ambapo raia wa Kenya wanasaidiana kipindi hiki cha janga kuhakikisha hatua zinachukuliwa bila kufuata urasimu

7.Afisa yeyote wa polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.

Image caption Jinsi chanjo ya conrona itakavyofanya kazi

Awali Bwana Kenyatta alisema , kwa mujibu wa agizo la kuepuka maeneo yenye mikusanyiko mikubwa, watu waepuke maeneo yenye umati wa watu, agizo lake likisema watu :

  • waepuke mikusanyiko ikiwemo maeneo ya kuabudu
  • wapunguze mikusanyiko ya kijamii mkiwemo harusi na mazishi, na masharti hayo yazingatiwe mara moja na wanafamilia
  • waepuke maeneo yenye msongamano wa watu mkiwemo maduka ya jumla na maeneo ya burudani
  • wapunguze mikusanyiko katika maeneo ya usafiri wa umma na kwingineko iwezekanavyo.
  • Kuwepo ukomo wa wageni wanaotembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali za umma na za kibinafsi.