Haki miliki ya picha Reuters Image caption Congo ilitangaza kuumaliza ugonjwa wa Ebola

Wakati maambukizi ya kwanza ya ugonjwa wa COVID-19 yalipothibitishwa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo mapema mwezi Machi, taifa hilo lilikuwa limetangaza kuwa liko huru na ugonjwa wa ebola kwa wiki kadhaa.

Ilidhaniwa kuwa vifaa tiba ambavyo vilitumika kukabiliana na ugonjwa wa ebola vingeweza kukabiliana na ugonjwa mpya wa corona.

Lakini Ijumaa, ikiwa ni siku mbili tu baada ya Shirika la afya duniani kutangaza mwisho wa mlipuko wa Ebola uliosababisha vifo zaidi ya 2,000, wagonjwa wengine waliripotiwa kupata maambukizi ya ebola mjini Beni mashariki mwa DRC

Wakati ugonjwa wa Corona ukisambaa nchini humo, mamlaka ya afya ambayo sasa kukabiliana na magonjwa yote mawili ya mlipuko hatari wakati wakiwahudumia wagonjwa wa mlipuko wa kipindupindu pia.

  • Mlipuko wa virusi vya corona waongezeka,lakini kwanini iwe hivyo?
  • Teknolojia 'njia mbadala' ya kutibu magonjwa
  • Jinsi mazishi ya waliokufa kwa corona yanavyoibua maumivu

Maambukizi ya Ebola, yalisambaa zaidi Mashariki mwa Congo tofauti na COVID-19 ambayo imesambaa katika mji mkuu wa Kinshasa,mpaka kwenye majimbo yenye mgogoro ambapo kuna wagonjwa 235 walioripotiwa kwa ujumla.

Wakati Ebola, ambayo bado haina kinga au tiba ambayo imethibitika kuwepo duniani kukabiliana na janga hilo.

Dunia sasa inakabiliana na janga hilohilo la kutafuta tiba au chanjo pamoja na msaada wa kuweza kukabiliana na ugonjwa wa mlipuko.

Mchanganyiko wa taarifa mbili kuhusu maambukizi mapya ya magonjwa yanayoambukiza barani Afrika, yameondoa imani ya watu kwa serikali zao kuwa na uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Kwa kuanzia katika hatua ya kusitisha mpango wa kufunga mji wa Kinshasa.

Haki miliki ya picha EPA Image caption Wahudumu wanaosaidia shughuli za maziko

Mikakati mipya ya kutoa jukumu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa watu wanafuata maagizo ni makosa ambayo yanairudia, wakati wa maambukizi ya corona.

"Baadhi ya njia hatari ya kukabiliana na anga hilo ni kuwa na kujiamini kupita kiasi kuwa waliweza kukabiliana na Ebola basi wataweza katika janga hili pia… ," alisema Tariq Riebl, afisa wa Umoja wa mataifa.

Aliongeza kuwa ugonjwa huu ni sawa na timu mbili tofauti.

Kuna changamoto ya Ufadhili

Kutokomezwa kwa ugonjwa wa Ebola kulileta matumaini kuwa baadhi ya rasilimali ambazo zilitumika kwa kipindi cha kipindi cha miezi 20 kuwatibu wagonjwa wa ebola, ikiwa ni pamoja na maabara, vifaa tiba na wataalamu wa afya ambao walielimishwa jinsi ya kukabiliana na magonjwa yanayoambukiza.

Mipango hiyo inabidi irejerewe tena katika suala la vituo vilivyokuwa vinatumika katika wagonjwa kutumiwa na waonjwa wa corona, visa vipya vinaonyesha kuwa vituo vya Ebola vinahitajika kufunguliwa tena ili kuwatibu wagonjwa wa ebola.

Maambukizi ya mwanaume mwenye miaka 26, yamepelekea utafiti kufanyika ili kubaini maambukizi ya Ebola, aliyapata wapi.

Kipindi ambacho mtu aliyekufa na Ebola kutangazwa nchini humo ilikuwa Februari 17,kufanya mnyororo wa maambukizi ambayo hayajafahamika kutiliwa shaka.

Hata kama hawatapatikana , sasa watahitaji siku 42 ambazo ni mara mbili ya siku 21-ambazo walikuwa wanakaa awali kabla ugonjwa huo haujatangazwa kuisha.

Wakati mamilioni ya fedha yakiwa yametumika kupambana na Ebola, sasa hakuna ufadhili wa kutosha , ufadhili unatolewa kwa mujibu wa shirika la afya duniania WHO, ambapo dola milioni 20 zinahitajika kutumika kukabiliana na majanga yote.

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo , imeweka bajeti ya dola milioni 135 kukabiliana na ugonjwa huo, kwa kuangalia ukubwa wan chi na idadi ya maambukizi kuwa kubwa zaidi ya maambukizi ya Ebola - lakini ufadhili ni mdogo kutoka nje na ndani ya nchi.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Mhudumu wa afya

Ingawa baadhi ya ufadhili wa Ebola ulitumika kujenga majengo mapya ya huduma za afya, wafanyakazi wa msaada wametoa angalizo kuwa ni kiwango kidogo cha ufadhili kiliwekezwa kwenye sekta hiyo ya afya, na kufanya kuwa ni vigumu kuakabiliana na mlipuko huu mpya.

Kuna maabara moja tu mjini Kinshasa yenye rasilimali ambazo zinahitajika katika taifa hilo ambapo sampuli zapatazo ya milioni 80 zinahitajika, ndio maana kuna ucheleweshaji wa upatikanaji wa majibu ya vipimo.

"Fedha iliyokuja kwa ajili ya Ebola, lakini ilitumika zaidi na asasi zenyewe na hazikuweza kusaidia sekta ya afya kitaifa.

Makundi ya msaada yanasema kuwa yako tayari kusaidia taifa hilo kukabiliana na janga jipya la ugonjwa wa maambukizi .

- Baadhi wakiwa tayari katika programu lakini changamoto ni mipaka kufungwa, hivyo inawawia vigumu kutuma wataalamu wao.

"Wakati wa Ebola, zaidi ya mamilioni ya dolla yalitolewa, visa zaidi ya 3,000-na maelfu ya wafanyakazi walitumwa kuja kupambana na ugonjwa huo," alisema Riebl wa UN. "Kwa upande wa virusi vya corona, tatizo halipo Kongo peke yake hivyo ni ngumu kutuma nguvu kazi ya kiasi hicho".

Ujumbe uliochanganyika

Ingawa congo ina uzoefu wa kushughulikia mlipuko wa Ebola mara nne, lakini mlipuko wa sasa unakuja wakati ambao Ebola unakuwa ugonjwa wa pili dunian kuambukiza.

Makundi ya kutoa misaada yanasema kuwa mlipuko wa ebola umekuwa somo kwa mlipuko wa virusi vya corona, haswa katika umuhimu wa kuhakikisha kuwa jamiii na wafanyakazi wa afya wanapewa kipaumbele.

Mashirika ya msaada wa kibinadamu yanatarajiwa kuchukua hatua kukabiliana na virusi hivi , ambapo sasa serikali zinakabiliana na janga hilo katika mji mkuu.

"Hali hii ya corona ni tofauti na itatufanya tuone ufanyaji kazi tofauti na wakati wa mlipuko wa Ebola," alisema Dr. Rigo Fraterne Muhayangabo, Mkurugenzi wa International Medical Corps nchini Congo. "Kuna matumaini kuwa hatutaona matokeo yanayofanana na wakati uliopita."

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Mji mkuu Kinshasa ulifungwa kuzuia maambukizi ya virusi

Lakini dalili za kutoiamini serikali tayari zimeanza kujitokeza.

Wananchi wengi waliamini kuwa wakati wa mlipuko wa Ebola ulikuwa wakati wa kupata fedha, na sasa wasiwasi huo huo uko miongoni mwa wafanyakazi wa mashirika ya usaidizi.

Wakati mamlaka ilipotangaza mgonjwa wa kwanza kuwa na corona kuwa alikuwa ametokea ughaibuni mwezi Machi, walieleza taifa alilotokea tofauti , taifa lake tofauti na hata karantini aliyokuepo haikuwa ya kweli, kila taarifa haikuwa ya kweli kuhusu mgonjwa huyo wa kwanza.

Hali ambayo haikusaidia na zaidi ilileta mchanganyiko wa watu, wa mji wa Kinshasa ambao una watu wapatao milioni10 na wakati ambao waliamua kusitisha kufunga mji huo mara baada ya amri ya katazo la kutoka nje kutangazwa.

  • Coronavirus: Kwa nini ni hatari kugusa uso wako
  • Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona
  • Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus
  • Je unaweza kupata coronavirus mara mbili?

Amri ya kufunga mji wa kibiashara wa Kinshasa wiki iliyopita ulitaka kuanzishwa katika miji ya mashariki ya Beni na Butembo.

Lakini makundi ya haki za binadamu yamekosoa namna ambavyo bara la Afrika linakabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa ,kutumia nguvu.

Wakati wa mlipuko wa Ebola askari na polisi walitumika kutumia katika vituo vya matibabu na sasa corona askari awanatumika zaidi.

Askari wameuwa watu wapatao watatu nchi humo katika harakati za kukabiliana na ugonjwa huu mpya, mwishoni mwa Machi kwa mujibu wa UN ambao walizungumza na shirika la Human Rights Watch (HRW), wakati madereva wa pikipiki mjini Beni walisema kuwa askari walikuwa wanawapiga kwa kutofuata utaratibu wa makatazo ya usafirinyaliyowekwa.

Suala la usalama

Hofu ya hali ya kiusalama haswa katika eneo la mashariki ya Kongo ambalo lina migogoro.

Vurugu katika ukanda huo, ramani zinaonyesha kuwa waasi wamesitisha mashambulizi kutokana na maambukizi haya hivyo kama vyombo vya usalama vitahusishwa na mapambano ya magonjwa haya, hali inaweza kubadilika.

Serikali imewakata makundi makundi ya upiganaji pamoja na operesheni ambazo askari walikuwa wanazifanya zisimame.

Huko Beni, eneo ambalo ugonjwa wa Ebola umeacha familia nyingi simanzi na yatima kuwa wengi, watoto wanahangaika na bei za juu za chakula ambazo zimepanda sokoni kutokana na mlipuko wa corona.

Wakati huu wa mlipuko, maskini wanazidi kuwa maskini na kuhangaika zaidina na wanaweza kuwaunga mkono waasi kutokana na hali ngumu ya maisha.